Wapiganaji wa Hamas walipofanya uvamizi wa kigaidi ndani ya Israel, waliuwa watu 1,200 na kuwateka wengine takriban 240.
Takriban 105 kati ya hao wameachiliwa huru tangu uvamizi wa Oktoba 7 lakini wengi bado wanashikiliwa mateka na wapenda wao wanaendelea kuwakosa.
Jimmy Miller, Jamaa wa Mateka anaeleza: “Nimefungwa bila ya chakula, bila ya umeme, bila ya maji, bila ya misaada yoyote ya kibinadamu.”
Mashambulizi ya Angani Gaza
Operesheni za kijeshi za anga na ardhini za Israel huko Gaza, ambazo zinalenga kuliharibu kundi la wanamgambo, wamewaua takriban Wapalestina 24,000, asilimia kubwa ya hao ni wanawake na watoto, kwa mujibu wa wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza.
Zaidi ya asilimia 85 ya watu milioni 2.3 huko Gaza wamekoseshwa makazi. Miongoni mwao, Heba Bakr, ambaye ana uja uzito wa miezi sita.
Mpalestina Aliyekoseshwa Makazi
Heba Bakr, Mpalestina Asiyekuwa na Makazi anasema: “Nitapata mtoto. Nina wasi wasi kuhusu tarehe yangu ya kujifungua; nitajifungulia wapi? Watanishughulikia vipi wakati wa kujifungua? Wataanza vipi kunipatia matibabu wakati nikijifungua.”
Kutoka Vatican, Baba Mtakatifu Francis alitoa tena wito wake wa amani akisema: “Vita vyenyewe ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Watu wanahitaji amani; duniani inahitaji amani.”
Maandamano Rome, London na Washington
Maandamano yamefanyika Rome, London na Washington mwishoni mwa wiki, pia wakitaka kumalizwa kwa vita, lakini Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hakubali kusalimu amri kwa shinikizo la umma.
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel alikuwa na haya ya kusema: “Wakati huu, kinachokuja kwanza ni kusughulikia gharama ya vita, na kuturuhu sisi kuendeleza vita katika mwaka unaokuja na kuvikamilisha, ikiwemo kulitokomeza kundi la Hamas, ikiwemo kuwarejesha mateka wetu.”
Siku ya Jumamosi, Osama Hamdan, afisa mwandamizi wa Hamas, ambaye kundi lake limetajwa na Marekani kuwa ni kundi la kigaidi, alisema mateka wanahudumiwa vizuri. Pia alizungumzia makubaliano ambayo Israel imesema imeyafikia na Qatar kufikisha dawa kwa mateka.
Osama Hamdan, Afisa Mwandamizi wa Hamas alieleza kuwa: “Tuko makini sana kuwatendea vizuri, lakini tutawahudumia kwa kila dawa tuliyonayo ambayo pia inawafikia watu wetu, na hapa tunashukuru kaka zetu huko Qatar ambao walichukua jukumu la kupeleka dawa.”
Nini Hatma ya Mzozo huo?
Bila ya kuwepo na mwisho kwa mzozo huu, wale wanaoshikiri mikutano ya hadhara mjini Tel Aviv wamesimama kimya kwa sekunde 100 jana Jumapili, wakiwakilisha idadi ya siku ambazo mateka wameshikiliwa. Kusimama kwa muda kwa harakati za kiraia na kibiashara pia kulitangazwa na shirikisho la umoja wa wafanyakazi huko Israel kuadhimisha alama kuu katika vita.
Ripoti ya mwandishi wa VOA Veronia Balderas Iglesias.
Forum