Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 10:57

Russia yaitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la UN, ili kuzungmzia mashambulizi ya Marekani dhidi ya Yemen


Ndege ya kijeshi ya Uingereza ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa RAF Akrotiri nchini Cyprus, ikielekea kufanya mashambulizi ya Yemen. Jan. 11, 2024.
Ndege ya kijeshi ya Uingereza ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa RAF Akrotiri nchini Cyprus, ikielekea kufanya mashambulizi ya Yemen. Jan. 11, 2024.

Russia imesema kwamba imeitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Ijumaa, ili kuzungumzia mashambulizi ya kijeshi kwa Yemen kutoka kwa Marekani na Uingereza.

Marekani na Uingereza wameanzisha mashambulizi ya anga na baharini, dhidi ya malengo ya Houthi nchini Yemen, yakiwa ni majibu kwa mashambulizi dhidi ya meli kwenye bahari ya Shamu, hatua inayoonekana kama kuenea kikanda kwa vita vya Israel na Hamas huko Gaza.

Msemaji wa kundi la kihouthi amesema kwamba mashambulizi ya Marekani na Uingereza hayana uhalali, na kwamba kundi hilo linaloungwa mkono na Iran litaendelea kushambulia meli zinazoelekea Israel.

Kamandi ya Marekani imesema Alhamisi jioni kwamba mashambulizi hayo yalilenga zaidi ya malengo 60 kwenye maeneo 16 katika eneo linalodhibitiwa na wa Houthi ndani ya Yemen. Mashambulizi hayo yanasemekana pia kushirikisha Australia, Canada, Netherlands na Bahrain.

Forum

XS
SM
MD
LG