Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:22

Siku 100: Mapigano makali yanaendelea katika miji ya mashariki ya Ukraine


A woman runs from a house that's on fire after shelling in Donetsk, on territory under control of the Donetsk People's Republic, in eastern Ukraine, June 3, 2022.
A woman runs from a house that's on fire after shelling in Donetsk, on territory under control of the Donetsk People's Republic, in eastern Ukraine, June 3, 2022.

Mapigano makali yanaendelea katika miji muhimu ya mashariki mwa Ukraine katika siku ya 100 ya vita vya  Russia, huku pande zote Moscow na Kyiv zikidai zimepata mafanikio katika uwanja wa mapambano.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema Ijumaa kuwa majeshi ya Russia yamefanikiwa katika jukumu lao kubwa lililoelezwa la “kuwalinda raia” katika maeneo yanayoshikiliwa na wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine.

FILE PHOTO: Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov
FILE PHOTO: Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov

Aliongeza kuwa majeshi ya Russia “yamekomboa” baadhi ya maeneo ya Ukraine na kwamba “zoezi hili litaendelea mpaka malengo yote ya operesheni maalum ya kijeshi yamefanikiwa.”

Majeshi ya Russia yamekuwa yakijaribu kuizingira miji ya Sievierodonetsk na Lysychansk huko katika mkoa wa Luhansk lilioko mashariki mwa Ukraine.

Mkuu wa mkoa wa Luhansk chini ya utawala wa Ukraine, Serhiy Gaidai, ameiambia televisheni ya taifa Ijumaa kuwa Ukraine ilikuwa imelikamata tena eneo kubwa la Sievierodonetsk. Alisema majeshi ya Ukraine yalikuwa yamechukua tena kiasi cha asilimia 20 ya eneo ambalo lilitekwa na Russia.

Gaidai alisema kuwa wanajeshi wa Russia wamekuwa wakipiga hatua kwa kutumia silaha nzito, na mara Ukraine itakapokuwa na silaha za masafa marefu za kutosha kutka Magharibi, itakuwa na uwezo wa kuwayafurusha majeshi ya Russia.

Marekani na Uingereza zimeahidi wiki hii kutuma mfumo wa makombora ya kisasa kwa Ukraine. Wizara ya Ulinzi ya Ukraine ilisema Ijumaa kuwa wanajeshi wake tayari wameanza mafunzo huko Ulaya namna ya kutumia silaha hizo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika hutoba yake kwa njia ya video Ijumaa, “Tayari tumeweza kuihami Ukraine kwa siku 100,” akiongeza, “Ushindi utakuwa wetu.”

Katika tamko lake Ijumaa kuhusu siku 100 za uvamizi huo, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema, “Mgogoro huu tayari umegharimu maisha ya maelfu ya watu, umesababisha uharibifu usioelezeka, umesababisha mamilioni ya watu kukimbia makazi yao, na matokeo yake ni ukiukaji wa haki za binadamu usiokubalika na kuchochea migogoro ya aina tatu – Chakula, nishati na fedha – unawasukuma zaidi walio katika mazingira hatarishi, nchi na uchumi.”

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres

Guterres alisema, “Kwa haraka zaidi pande zinazohusika zijihusishe kwa nia njema katika juhudi za kidiplomasia ili kumaliza vita hivi, ni jambo zuri kwa ajili ya Ukraine, Russia na dunia. Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia juhudi kama hizi.”

Habari hii imechangiwa na mashirika ya habari ya AP na Reuters

XS
SM
MD
LG