Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:12

Maafisa 65 wa ngazi ya juu wa Russia wawekewa vikwazo vipya


Vifaru vya jeshi la Russia nchini Ukraine June 2, 2022. PICHA: REUTERS
Vifaru vya jeshi la Russia nchini Ukraine June 2, 2022. PICHA: REUTERS

Umoja wa ulaya umetangaza vikwazo vipya dhidi ya maafisa wakuu wa jeshi la Russia, wanaodaiwa kusimamia mauaji yanayoendelea nchini Ukraine, wakiwemo makamanda wa jeshi wanaoshutumiwa kwa mauaji katika miji ya Bucha n a Mariupol, inayoshikiliwa na Russia.

Umoja wa ulaya umeweka vikwazo kwa mali za watu 65, pamoja na kuwawekea vizuizi vya usafiri.

Umoja huo sasa umewalenga watu 1,160, akiwemo rais Vladimir Putin, watu wanaouunga mkono utawala wa Russia pamoja na maafisa wengine wa ngazi ya juu, kuhusiana na mchango wao wa uchokozi ndani ya Russia tangu mwaka 2014.

Kanali Azatbek Omurbekov na kanali generali Mikhail Mizintsev, ambao wanajulikana kama wauaji wa Mariupol, ni miongoni mwa watu waliowekewa vikwazo vya hivi punde.

Makamanda hao wanashutumiwa kwa kuongoza mauaji, unajisi na ukandamizaji wa watu wa Bucha, nje ya mji wa Kyiv.

Mkuu wa sera za nje katika umoja wa ulaya Josep Borrell amesema kwamba uhalifu wa kivita hauwezi kuvumiliwa.

XS
SM
MD
LG