Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 16:56

Russia yashutumiwa kwa wizi wa nafaka ya Ukraine


Rais wa RussiaVladimir Putin. May 22 2022. PICHA: REUTERS
Rais wa RussiaVladimir Putin. May 22 2022. PICHA: REUTERS

Balozi wa Ukraine nchini Uturuki amesema kwamba nafaka inayouzwa nchini humo imeibwa na Russia kutoka Ukraine, akiongezea kwamba ameomba msaada wa Uturuki kutambua na kuwakamata watu wanaoiba nafaka hiyo na kuisafirisha.

Balozi Vasyl Bodnar, amesema kwamba Russia inasafirisha nafaka iliyoibwa kutoka Ukraine, na kuongezea kwamba utawala wa Kyiv unashirikiana na polisi wa kimataifa –Interpol, kuwakamata wahusika.

Ubalozi wa Ukraine mjini Ankara imetaja meli zinazosafirisha chakula cha wizi kutoka Ukraine. Meli hizo ni Nadezhda, Finikia, Sormivskiy, Vera, na Mikhail Nenashev.

Ubalozu wa Ukraine mjini Beirut, umesema kwamba Russia imetuma tani 100,000 za ngano iliyoibwa kwa Syria, ambayo ni mshirika wake wa karibu.

XS
SM
MD
LG