Ukame wa Muda mrefu pamoja na huduma dhaifu za afya kutokana na ukosefu wa uthabiti, janga la COVID 19, na ukosefu wa fedha vimesababisha zaidi ya watu milioni moja kuhitaji msaada wa haraka wa lishe kote somali, Oromia, SNNP na maeneo ya upande wa magharibi.
Hata hivyo hali mbaya ya utapiamlo inatarajiwa katika miezi ya hivi karibuni wakati bei ya vyakula inazidi kuongezeka kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu ya Ethiopia na vita vya Ukraine, huku mifugo ya familia ikiendelea kushuka thamani kutokana na ukame mkubwa katika historia kwenye pembe ya Afrika kuwahi kutokea.
Katika eneo la Somali mashariki mwa Ethiopia moja ya eneo lililoharibiwa vibaya na ukame, kiwango cha utapiamlo kwa zaidi ya miezi 12 kimeongezeka kufikia asilimia 64 ikiwa ni ongezeko la asilimia 43 kati ya mwezi januari na april pekee.