Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 22:18

Zaidi ya watu 4500 wamekamatwa Ethiopia


Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Zaidi ya watu 4,500 wameripotiwa kukamatwa katika mazingira ya kutatanisha nchini Ethiopia katika siku za karibuni.

Watu hao wamekamatwa katika eneo la Amhara kati ya tarehe 23 mwezi May hadi sasa, na wanaharakati wanasema huenda idadi kamili ya waliokamatwa ikawa ya juu kuliko inavyoripotiwa.

Miongoni mwa watu ambao wamekamatwa ni wanaharakati, waandishi wa habari na watu wanaodaiwa kuwa wakosoaji wa serikali.

Wanaharakati wanaishutumu serikali ya Ethiopia kwa kuwalenga watu kutoka jamii ya Amhara, inayodaiwa kuwa tishio kwa utawala wa sasa, baada ya vita vya Tigray.

Kabila la Amhara ni la pili kwa ukubwa baada ya Tigray, nchini Ethiopia.

Baraza huru la kutetea haki za kibinadamu nchini Ethiopia limesema kwamba haijulikani mahali ambapo watu wanaokamatwa wanazuiliwa, na kudai kwamba watu wengi wametekwa nyara.

XS
SM
MD
LG