Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 22, 2025 Local time: 03:09

Shambulizi la kujitoa muhanga Somalia laua 10, kujeruhi 15


Shambulizi la kigaidi Somalia
Shambulizi la kigaidi Somalia

Takriban watu 10 wameuawa huku wengine 15 kujeruhiwa Jumapili kwenye shambulizi la kujitoa muhanga la kwenye gari katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Gari hilo lilikuwa kwenye msongamano wa magari kwenye barabara yenye shughuli nyingi ya Maka Al Mukarama.

Mwanadishi wa VOA idhaa ya kisomali alitembelea eneo la tukio na kusema kuwa mshambuliaji alitegua vilipuzi baada ya kukwama kwenye msongamano kwa muda mrefu, kutokana na ukaguzi uliokuwa ukifanywa na maafisa wa usalama.

Wengi walioathiriwa walikuwa wanatoka kwenye duka karibu na barabara hiyo.

Afisa wa usalama ambaye hakutaka kutambulishwa amasema inaaminika kuwa gari hilo lilikua likielekea kwenye jengo la bunge ambako wabunge walikuwa wakijadili maswala ya kikatiba.

XS
SM
MD
LG