Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 18:17

Uganda yathibitisha al Shabaab imeua wanajeshi wake 12


Askari wa jeshi la Somalia wakifanya shambulizi katika maficho ya al-Shabaab
Askari wa jeshi la Somalia wakifanya shambulizi katika maficho ya al-Shabaab

Wapiganaji wa Al Shabaab nchini Somalia Jumapili wamewaua wanajeshi 12 wa Jeshi la Uganda (UPDF) katika shambulizi la ghafla dhidi ya vikosi vya Umoja wa Afrika upande wa kusini wa nchi hiyo.

Waasi hao wamedai kuwa wamewaua wanajeshi 39 wa vikosi vya Umoja wa Afrika katika shambulizi la kushitukiza kwenye eneo hilo.

Taarifa iliyotolewa Jumatatu na Brigedia Richard Karemire, msemaji wa UPDF amethibitisha kuwa patroli ya pamoja iliyofanywa na jeshi la Somalia (SNA), Vikosi vya Umoja wa Afrika vya UPDF chini ya kikosi cha 7 cha wapiganaji wa kundi la 22 kilivamiwa na magaidi wa al Shabaab.

“Kutoka katika uwanja wa vita, imethibitishwa kuwa UPDF imepoteza askari wake wenye nidhamu 12 na wengine 7 kujeruhiwa. Miili ya askari hao na ile ya wale waliojeruhiwa imepelekwa kwenye hospitali ya daraja la pili Mogadishu kwa matibabu na kufanyiwa taratibu zinazotakiwa,” Brig Richard Karemire amesema katika taarifa yake.

Ameongeza kusema kuwa: “Ofisi ya UPDF ya Utumishi na Uongozi inaendelea kufanya mawasiliano na warithi wa marehemu hao na ndugu za wale waliojeruhiwa kuwafahamisha kile kinachoendelea katika maandalizi ya kuisafirisha miili ya marehemu hao kwenye maeneo ya makazi yao kwa ajili ya maziko.”

XS
SM
MD
LG