Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:17

Mkurugenzi IEBC Kenya akutwa amekufa


Chris Musando
Chris Musando

Mkurugenzi wa ICT, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya, Chris Musando, ambaye alitoweka siku ya Ijumaa amkutikana amekufa.

Polisi Jumatatu wamesema kuwa mwili wake na ule wa mwanamke ambaye hakuweza kutambulika iligunduliwa katika eneo la Kikuyu, Kaunti ya Kiambu, na kupelekwa kwenye sehemu ya kuhifadhi maiti jijini.

Wahudumu wa sehemu ya kuhifadhi maiti wameliambia gazeti la the Nation kwamba miili hiyo ililetwa Jumapili saa 11am.

Miili hiyo, walisema kuwa ililetwa na polisi ikiwa imebebwa katika gari yao na Musando alikuwa amesajiliwa kama “mtu asiyejulikana”.

Wanafamilia wa marehemu Musando walikwenda kwenye sehemu ya kuhifadhi maiti na kuutambua mwili wake.

XS
SM
MD
LG