Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 21:02

John Kerry kuongoza waangalizi katika uchaguzi wa Kenya


Mwanamke raia wa Kenya akiondoka kwenye kitu cha kuandikisha wapiga kura mjini Nairobi, Desemba 2012.
Mwanamke raia wa Kenya akiondoka kwenye kitu cha kuandikisha wapiga kura mjini Nairobi, Desemba 2012.

Marekani itakuwa nchi ya kwanza kutuma waangalizi kufuatilia uchaguzi mkuu wa Kenya unaopangwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu.

Ujumbe wa waangalizi 80 walioteuliwa na kituo cha Carter wakiongozwa na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry unatarajiwa kuwasili nchini Kenya wiki hii.

Miongoni mwa waangalizi hao kutoka nchi 34 ni pamoja na aliyekuwa waziri mkuu wa Senegal, Amiata Toure.

Tangu Aprili mwaka huu waangalizi wamekuwa wakifuatilia matayarisho ya uchaguzi huo katika kaunti mbali mbali nchini Kenya.

Miezi miwili iliyopita rais wa Marekani Donald Trump aliteua kamati ya watu kumi kuongoza waangalizi watakaofuatilia uchaguzi mkuu wa Kenya.

“Ulimwengu mzima unasubiri kuona jinsi Kenya itakavyofanya uchaguzi wake Agosti”, alisema rais Trump alipokutana na wakuu wa bunge la Ulaya katika halfa iliyoandaliwa huko White-House.

Ripoti iliyotolewa wiki hii na kituo cha Carter iliisifu tume ya uchaguzi nchini Kenya kutokana na mikakati iliyoweka kusimamia uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Kituo hicho pia kiliteuwa waangalizi kufuatilia uchaguzi mwingine uliofanyika mapema mwaka 2013, na kutoa ripoti iliyosema serikali ya Kenya ilijitahidi katika kuhakikisha uchaguzi ni wa kidemokrasia.

Lakini waangalizi hao walikosoa mirengo ya kisiasa iliyoongozwa na wanasiasa mashuhuri, rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga.

XS
SM
MD
LG