Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 12:30

Shambulizi la kigaidi lajeruhi polisi 5 Kenya

Polisi wa Utawala nchini Kenya wamegundua bomu (IED) lililokuwa limezikwa ardhini katika kaunti ya Garissa.

Muda mfupi baada ya kutokea shambulizi ambalo liliwajeruhi polisi wa utawala 5 Garissa, bomu hilo liligunduliwa wakati polisi walipokuwa wako katika harakati za kupambana na watu hao ambao wanadaiwa kuwa ni magaidi.

Mwandishi wetu nchini Kenya amesema baada ya bomu hilo kugunduliwa, maafisa wa Jeshi la Kenya (KDF) waliitwa kuja kulitegua.

Katika pambano hilo kati ya polisi na magaidi hao polisi waliweza kuwasambaratisha watu hao na kurejesha utulivu katika eneo hilo.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Hubbah Abdi, Kenya

Pandisha zaidi

Makundi

XS
SM
MD
LG