Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 23:07

Shambulio la kigaidi lauwa watu 10 Niger


Wakazi wakusanyika kwenye eneo la shambulizi katika kijiji cha Solhan Burkina Faso Burkina Faso Juni 7, 2021. Burkina Faso Prime Minister's Press Service/Handout via REUTERS
Wakazi wakusanyika kwenye eneo la shambulizi katika kijiji cha Solhan Burkina Faso Burkina Faso Juni 7, 2021. Burkina Faso Prime Minister's Press Service/Handout via REUTERS

Vyombo vya habari nchini Niger vinaripoti karibu watu 10 wameuliwa kutokana na shambulio la kigaidi kaskazini mwa nchi.

Maafisa katika jimbo la Tillaberi wanasema wanamgambo walitumia pikipiki kufanya mashambulio yao kwenye vijiji viwili vya Danga Zouani na Korombara pamoja na wakazi wa mashamba yaliyoko karibu na vijiji.

Wanamgambo hao walichoma moto maduka ya nafaka na nyumba za watu.

Tilaberi inapatikana kwenye ncha ya mpaka kati ya Niger, Burkina Faso na Mali sehemu inayofahamika kwa mashambulizi ya mara kwa mara.

Mamia ya watu wameuliwa na maelfu kulazimika kukimbia kutoka makazi yao katika kanda ya Sahel kutokana na mashambizi hayo yanayofanywa na wanamgambo wanaofuata itikadi kali za kidini.

Habari hii inatokana na vyanzo vya habari mbalimbali

XS
SM
MD
LG