Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:42

Kiongozi mpya wa Chad yupo Niger kwa mazungumzo yanayohusu usalama na Rais Bazoum


Kiongozi mpya wa Chad, Mahamat Idriss Deby
Kiongozi mpya wa Chad, Mahamat Idriss Deby

Wanajeshi wapatao 1,200 wa Chad wamepelekwa  magharibi mwa Niger karibu na mpaka wa Burkina Faso mahala ambako mashambulizi ya wenye msimamo mkali yameongezeka katika miaka michache iliyopita

Kiongozi mpya wa Chad, Jenerali Mahamat Idriss Deby alisafiri kwenda Niger Jumatatu ikiwa ni safari yake ya kwanza ya kimataifa tangu jeshi lilipomuweka madarakani mwezi uliopita kufuatia kifo cha baba yake.

Deby aliwasili katika mji mkuu wa Niger, Niamey mahala ambapo alilakiwa na waziri mkuu wa Niger, Ouhoumoudou Mahamadou na viongozi wengine. Kiongozi huyo wa Chad mwenye umri wa miaka 37, anatarajiwa kukutana na Rais mpya wa Niger, Mohamed Bazoum.

Wanajeshi wapatao 1,200 wa Chad wamepelekwa magharibi mwa Niger karibu na mpaka wa Burkina Faso, mahala ambako mashambulizi ya wenye msimamo mkali yameongezeka katika miaka michache iliyopita.

Chad na Niger wote ni wanachama wa G5 Sahel, kikosi cha usalama katika eneo kinachopambana na uasi, ikishirikiana na Burkina Faso, Mali na Mauritania.

XS
SM
MD
LG