Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:41

Mwakilishi maalum wa UN atembelea kambi ya wakimbizi Burkina Faso


Mcheza filam wa Marekani Angelina Jolie, ambaye ni mwakilishi maalum wa UNHCR, akitoa taarifa kwenye kambi ya wakimbizi ilyo na wakimbizi 11,000 wa Mali kaskazini mwa Burkina Faso.
Mcheza filam wa Marekani Angelina Jolie, ambaye ni mwakilishi maalum wa UNHCR, akitoa taarifa kwenye kambi ya wakimbizi ilyo na wakimbizi 11,000 wa Mali kaskazini mwa Burkina Faso.

Mwigizaji wa Hollywood Angelina Jolie Jumapili alitembelea kambi ya wakimbizi huko Burkina Faso inayohifadhi wakimbizi wanaokimbia ghasia za wanajihadi nchini Mali, na kuipongeza nchi hiyo kwa kuwakaribisha waliokimbia makazi yao licha ya rasilimali chache na kupambana na uasi wake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Burkina Faso, kama majirani zake Niger na Mali, inasikitishwa na mashambulizi makali ya wanamgambo wanaohusishwa na al Qaeda na Islamic State ambayo yameua maelfu na mamilioni ya wakimbizi katika nchi hizo tatu.

Niko hapa kuonyesha mshikamano wangu kwa watu wa Bukinabe ambao wanaendelea kuwakaribisha ndugu zao kaka na dada waliokimbia makazi yao licha ya mashambulizi mabaya na changamoto, wakikubali kugawana kidogo walicho nacho wakati nchi nyingine zilizo na zaidi zimefunga mipaka yao na akili zao kwa wakimbizi, Jolie alisema.

Safari yake ilikuwa ya kuadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani, ambayo hufanyika kila mwaka Juni 20.

XS
SM
MD
LG