Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:52

Serikali - Tanzania yafuta leseni za kuhodhi maeneo ya madini


Professor Idris Kikula
Professor Idris Kikula

Serikali ya Tanzania imefuta leseni zote za kuhodhi maeneo ya madini na wamiliki wake wametakiwa kuomba upya wakizingatia Sheria ya Madini na kanuni zake.

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini, Profesa Idris Kikula amesema tangazo la Serikali namba moja la mwaka 2018 limesema maeneo yote yaliyopewa leseni yanarejeshwa serikalini bila hakikisho la kupewa tena.

Amesema hatua hiyo ni kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ikisomwa na marekebisho yake ya mwaka 2017 na kanuni ya 21 ya kanuni za Madini (Haki Madini 2018).

Amesema leseni zilizofutwa na wamiliki wake wanatakiwa kuomba tena na zinazihusu kampuni 11. Pia leseni hizo zinajumuisha migodi ya kati na mikubwa.

Migodi hiyo ni pamoja na Kabanga Nickel Company Limited, National Mineral Development Corporation Limited, Bafex Tanzania Limited ambayo inamiliki leseni za maeneo matatu.

Nyingine ni Mabangu Mining Limited, Resolute (Tanzania) Limited, Wigu Hill Mining Company Limited, Nachingwea Nickel Limited na Precious Metals Refinery Company Limited.

XS
SM
MD
LG