Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 20:08

Serikali kukagua mabwawa yote nchini Kenya


Mtoto akiwa ndani ya nyumba iliyobomoka baada ya kukumbwa na mafuriko yaliosababishwa na kupasuka kwa Bwawa la Patel

Mabawa yote nchini Kenya yatafanyiwa ukaguzi kufuatia tukio la kupasuka kwa Bwawa la Patel ambalo mpaka sasa limeuwa zaidi ya watu 40 katika eneo la Solai, Kaunti ya Nakuru.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Simon Chelugui amesema Jumamosi mabwawa hayo yatakaguliwa ili kuhakikisha kuwa hayahatarishi maisha ya watu.

Waziri huyo amesema baadhi ya mabwawa yalikuwa yamejengwa wakati wa ukoloni na serikali ya kitaifa itafanya kazi na kaunti mbalimbali kuyakagua ili kuhakikisha yako salama, vyanzo vya habari nchini humo vimeeleza.

“Tutatuma wataalamu na wahandisi kukagua malighafi iliyotumika kujengea mabwawa, kuangalia iwapo yalikuwa yamejengwa katika njia za maji, na iwapo wahandisi waliosimamia kazi hiyo ya ujenzi walikuwa wanaleseni za kufanya kazi hizo. Hatutaki kuona maafa mengine zaidi yanatokea,” amesema Chelugui.

Chelugui amesema hayo wakati anatembelea Bwawa la Patel lililosababisha vifo.

Bwawa hilo, lililokuwa limejengwa katika shamba la kahawa, lilipasuka Jumatano usiku na kuruhusu maji zaidi ya litre milioni 70 kusababisha mafuriko na kuharibu kabisa kila kitu kilichokuwa katika Kijiji.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG