Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 02:19

Serikali Kenya yapiga marufuku maandamano


Upinzani Kenya ukiandamana kupiga Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Jumatano Octoba 11, 2017

Wakati vyama vya upinzani nchini Kenya vikiahidi kufanya maandamano wakidai kuwepo mabadiliko kabla ya marejeo ya uchaguzi wa urais kufanyika, serikali imepiga marufuku maadamano katika miji mikuu mitatu.

Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang'i ametoa amri hiyo Alhamisi, akipiga marufuku maandamano katika wilaya za kati za kibiashara ikiwemo Mombasa, Kisumu, na makao makuu, Nairobi, akieleza kuwa “ni wazi, hivi sasa kuna ishara zote za uvunjifu wa amani.”

Miji hiyo mitatu ni ngome imara ya mgombea wa upinzani Raila Odinga, ambaye amesusia marejeo ya uchaguzi unaofanyika Octoba 26 kwa sababu Tume Huru ya Uchaguzi inayojulikana kama IEBC, haikuwabadilisha maafisa wake ambao anawalaumu kwa kusababisha kasoro nyingi katika uchaguzi uliopita.

Maelfu ya waandamanaji waliingia mitaani Nairobi Jumatano, siku moja baada ya Odinga kutangaza kuwa hatoshiriki katika marejeo ya uchaguzi.

Tume hiyo imesema Jumatano kuwa wagombea wote wanane kutoka kwenye uchaguzi wa awali wa Agosti watashiriki katika uchaguzi mpya.

IEBC imesema kuwa imepokea barua pekee kutoka kwa Odinga ikilalamika juu ya mfumo wa uchaguzi.

Kenya imeendelea kuwa njiapanda tangu matokeo ya uchaguzi ya awali ya yalipobatilishwa Septemba 1, kwa kile ambacho Mahakama ya Juu imesema ni “dosari na kukiukwa kwa sheria” wakati wa kupeperusha matokeo.Facebook Forum

XS
SM
MD
LG