Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 23:56

Senegal: Sonko aashiria nia ya kuvuruga uchaguzi iwapo hataruhusiwa kugombea


FILE PHOTO: Kiongozi wa upinzani wa Senegal Ousman Sonko.

Kiongozi wa upinzani wa Senegal, Ousmane Sonko, hana mpango wa kutafuta maridhiano, na Rais Macky Sall, na ameashiria kuwa anaweza kujaribu kuvuruga uchaguzi wa mwaka ujao, ikiwa hataruhusiwa kugombea, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha  France 24 siku ya Alhamisi.

"Hakutakuwa na uchaguzi katika nchi hii, iwapo Rais Macky Sall atapinga kugombea kwangu," Sonko alisema kutoka nyumbani kwake katika mji mkuu wa Dakar, ambako amekuwa chini ya kizuizi cha nyumbani, tangu alipohukumiwa kifungo cha miaka miwili, mwezi Juni, kwa mashtaka yaliyotokana na madai ya ubakaji.

Sonko amekanusha mashtaka hayo na kusema kuwa yanalenga kumzuia kushiriki katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Februari, mwakani.

Sonko, maarufu miongoni mwa vijana wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi, aliitisha maandamano kufuatia hukumu hiyo ya mwezi Juni.

Ghasia zilianza, ambapo maelfu ya waandamanaji walichoma majengo na magari, na kuwarushia mawe maafisa wa polisi, ambao walijibu kwa kurusha mabomu ya machozi na, baadhi ya mashahidi wanasema, risasi za moto.

Takriban watu kumi na sita walipoteza maisha yao.

Machafuko hayo yalichochewa, kwa kiasi kikubwa, na wasiwasi kwamba Sall angewania muhula wa tatu madarakani, katika uchaguzi wa mwezi Februari. Sall, tangu wakati huo amesema hatagombea.

Forum

XS
SM
MD
LG