Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:41

Marekani yampongeza rais wa Senegal kwa kutogombea tena urais


Rais wa Senegal Macky Sall alipomkaribisha raisi wa Uturuki Tayyip Erdogan ikulu iliyoko Dakar, terehe 28 Januari 2020. Picha na REUTERS/Zohra Bensemra.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amepongeza rais wa Senegal Macky Sall kwa kutangaza uamuzi wa kutogombania muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais utakaofanyika mwakani.

Rais Sall alitangaza uamuzi wake wakati wa hotuba yake kwa taifa kupitia kituo cha televisheni ya taifa, na kuuzima uvumi wa miaka kadhaa, ulozusha ghasia na wasiwasi wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

"Senegal ni kubwa kuliko mimi," alisema Sall katika hotuba ya Jumatatu, "imejaa watu wenye uwezo wa kuipeleka Senegal katika hatua nyingine."

Waziri Blinken alisema kwenye taarifa yake, "Tunaamini kuwepo kwa uchaguzi huru na wa haki na mabadiliko ya mamlaka yataimarisha taasisi zenye nguvu na nchi yenye utulivu na ustawi zaidi. Tamko la wazi la Rais Sall linaweka mfano katika kanda hiyo, tofauti na wale wanaotaka kuvuruga misingi ya kidemokrasia, pamoja na ukomo wa muda wa kuwepo madarakani.”

Sall alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2012, baada ya kumshinda rais aliyekuwa madarakani Abdoulaye Wade ambaye alikuwa akiwania muhula wake wa tatu. Sall alichaguliwa tena mwaka wa 2019 chini ya katiba iliyofanyiwa marekebisho ambayo iliweka kikomo cha raisi kuwepo madarakani kua mihula miwili ya miaka mitano - lakini wafuasi wake wamekua wakitoa hoji kuwa Sall anaweza kugombea muhula wa tatu kwa kuwa alichaguliwa chini ya katiba iliyopita.

Uvumi wa Sall kuweza kugombea tena mwaka 2024 ulizua maandamano yenye ghasia kote nchini mwezi uliopita, na kuzusha mapambano kati ya maafisa wa usalama na wafuasi wa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko ambapo watu 16 waliuawa. Ghasia hizo za mwisho zilitokea baada ya Sonko kupatiakana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono.

Uvumi huo pia ulitishia kuichafua sifa ya Senegal ambayo inajulikana kama kinara wa demokrasia na utulivu wa kisiasa katika kanda ya Afrika Magharibi yenye machafuko. Kanda hiyo imeshuhudia viongozi wakipuuza ukomo wa mihula uliowekwa na katiba na kubaki madarakani. Pamoja na kuwepo na mapinduzi ya kijeshi.

Baadhi ya taarifa za habari hii zinatola katika shirika la habari la AP, Reuters, AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG