Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 00:14

Rais wa Senegal ametangaza hatogombea muhula wa tatu madarakani 2024


Macky Sall, Rais wa Senegal.

“Hata kama nina haki, nilihisi kuwa wajibu wangu sio kuchangia kuharibu kile nilichojenga kwa ajili ya nchi hii” Sall alisema. “Nilisema kuwa mwaka 2019 ulikuwa ni muhula wangu wa mwisho. Najua kwamba uamuzi huu utakuja kama mshangao kwa wale wote ambao wana urafiki nami.

Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza Jumatatu kwamba hatogombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa mwaka ujao wa 2024, na kumaliza miaka kadhaa ya sintofahamu kuhusu mustakabali wake wa kisiasa ambao umepelekea kuchochea maandamano ya upinzani mwezi uliopita nchini mwake.

Mchambuzi wa siasa za kimataifa Amini Mwidau kutoka Canada anaelezea ujumbe huu unabadilisha vipi taswira ya siasa nchini Senegal.

Amini Mwidau mchambuzi wa siasa za kimataifa akizungumza na VOA Swahili.m4a
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:35 0:00

Katika hotuba yake iliyotumwa moja kwa moja kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook, Rais Sall alisisitiza kuwa katiba ya Senegal ingemruhusu kugombea kwake licha ya kuwa tayari ameshachaguliwa kwa muhula wa pili mwaka 2019.

“Hata kama nina haki, nilihisi kuwa wajibu wangu sio kuchangia kuharibu kile nilichojenga kwa ajili ya nchi hii” Sall alisema. “Nilisema kuwa mwaka 2019 ulikuwa ni muhula wangu wa mwisho. Najua kwamba uamuzi huu utakuja kama mshangao kwa wale wote ambao wana urafiki nami. Senegal ni zaidi ya mimi, imejaa watu wenye uwezo wa kuipeleka Senegal katika ngazi inayofuata.”

Mpinzani mkuu Ousmane Sonko kwa muda mrefu alikuwa amemtaka Rais Marky Sall kujiondoa katika uchaguzi wa mwaka 2024 akiishutumu serikali ya Sall kwa kupeleka kesi mahakamani dhidi ya kiongozi huyo wa upinzani katika juhudi za kukatiza ushindani kabla ya uchaguzi wa Februari.

Kumekuwa na hofu kubwa kwamba tamko la Sall kuhusu mustakabali wake wa kisiasa linaweza kuzusha wimbi jipya la machafuko katika taifa hilo la Afrika Magharibi ambalo kwa muda mrefu linatazamwa kama ngome ya utulivu katika eneo lenye machafuko ya kisiasa.

Forum

XS
SM
MD
LG