Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 09, 2023 Local time: 04:57

Salaam za Krismasi : Papa ahimiza mshikamano, ataka wakimbizi wasaidiwe


Papa Francis

Kingozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, katika sherehe za Krismasi, siku aliyozaliwa Yesu Kristo, amesema mwaka huu ni wa watu kushikamana pamoja, baina ya mataifa na tamaduni zake.

Katika ujumbe wake kwa jiji la Vatican na dunia nzima, papa alitoa nasaha hizo wakati akiongoza Misa ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa la Basilica mjini Vatican Jumanne.

“Maombi yangu ni muwe na Krismas yenye furaha, ni ombi langu la nyinyi kushikamana pamoja,” papa alieleza hilo wakati akihutubia zaidi wa Wakatoliki milioni moja duniani kote.

Ameongeza ni "ushirikiano kati ya watu wenye fikra mbalimbali, lakini wako tayari kuheshimu na kusikilizana; mshikamano kati ya watu wa dini mbalimbali."

Akielezea hisia zake juu ya bara la Afrika, Papa ameonyesha sikitiko lake kwa mamilioni ya watu ambao ni wakimbizi au wamelazimika kukimbia makazi yao na ambao wanahitaji misaada ya kibinadamu na pia kuhakikishiwa upatikanaji wa chakula.

Ameeleza hamu yake kuona migogoro ya silaha inamalizika ili kutoa fursa ya “chanzo kipya cha ushirikiano kufikia mabara yote duniani.”

Papa amesema naomba kwa Mungu Krismas hii iwawezesha watu kuunga udugu kwa jamii zote, Pia ni matarajio yake hili litaleta amani kati ya Waisraeli na Wapalestina, na huko Syria na Yemen, VOA imeripoti.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari papa amewakumbusha wananchi wa nchi zilizopiga hatua kimaendeleo kuishi maisha ya kawaida na kupunguza anasa.

Pia amekemea pengo kubwa lililopo duniani baina ya masikini na matajiri, na kutaka watu wayaenzi maisha ya Yesu aliye zaliwa kwenye umasikini, kwa kufuata nyayo zake.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG