Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 21:03

Rwanda yajikita katika maandalizi ya mkutano wa CHOGM


FILE PHOTO: Rais wa Rwanda Paul Kagame.
FILE PHOTO: Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Rwanda iko katika hali ya utata ikiwa inakaribia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Viongozi wa Serikali wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (Chogm) uliondaliwa kufanyika wiki ya Juni 23, wakati ikikabiliana na tuhuma mfululizo za jirani yake kuhusu kuingilia nchi hiyo.

Wakati matayarisho yakiwa yameshika kasi kabla ya mkutano huo, mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea kati yake na Jamhuri ya Kidemkorasia ya Kongo (DRC) unaweka dosari kabla ya tukio hilo, ukiwasukuma maafisa wa serikali kukanusha madai ya kuwa Kigali ina jukumu fulani katika ghasia mpya zinazoendelea.

Hadi hivi sasa majaribio ya kikanda ya kidiplomasia kuzima mivutano yanaonekana kushindwa wakati DRC ikitoa tuhuma mpya Jumatano kuwa Kigali imepeleka vikosi maalum vya wanajeshi 500 kuwasaidia waasi wa M23 ambao hivi karibuni walianzisha tena mashambulizi katika eneo la mashariki mwa DRC.

Kigali imekanusha na kutupilia mbali shutuma hizo.

Kigali, ambayo imesisitiza itaendelea kushikamana na mfumo wa kikanda katika kutatua mgogoro huu, pia inakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha mkutano wa Chogm unafanikiwa ambapo zaidi ya viongozi wa nchi 20 wamethibitisha kushiriki hadi sasa.

Juni 5, Rais wa Rwanda Paul Kagame alithibitisha utayari wa nchi hiyo kuwa wenyeji wa mkutano huo katika salamu za pongezi kwa Malikia Elizabeth II aliyekuwa akisherehekea utawala wake wa miaka 70.

“Wakati Rwanda ikijitayarisha kuwa wenyeji wa Chogm 2022, tunatarajia kuimarisha urafiki na ushirikiano ndani ya familia ya Jumuiya ya Madola,” Rais Kagame alituma ujumbe wa tweet.

Chanzo cha Habari Hii ni gazeti la The East African

XS
SM
MD
LG