Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:09

Wanajeshi wa Rwanda waliotekwa na jeshi la DRC waachiliwa huru

Watu 100,000 watoroka mapigano mashariki mwa Congo
Watu 100,000 watoroka mapigano mashariki mwa Congo

Wanajeshi wawili wa Rwanda waliotekwa na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi uliopita na kushutumiwa na mamlaka ya Congo kwa kuunga mkono mashambulizi ya waasi wameachiliwa huru, jeshi la Rwanda lilisema Jumamosi.

Congo ilisema wanajeshi hao wawili walizuiliwa ndani ya ardhi yake, ambapo walieleza kama ushahidi kwamba Rwanda inaunga mkono mashambulizi yanayoendelea yanayofanywa na waasi wa M23. Siku ya Alhamisi, iliongeza shutuma zake, ikiilaumu Rwanda kwa kutuma vikosi maalum 500 vilivyojificha mashariki mwa Congo.

Rwanda imekanusha kuhusika na mashambulizi ya M23 na kusema kuwa wanajeshi hao wawili walitekwa nyara na wanajeshi wa Congo ndani ya Rwanda.

Mzozo huo unaokua umeibua tena chuki za zamani kati ya majirani hao. Rwanda ilivamia mashariki mwa Congo mara mbili katika miaka ya 1990.

Mara kadhaa tangu wakati huo, wataalam wa Kongo na Umoja wa Mataifa wameishutumu kwa kuunga mkono wanamgambo mashariki mwa Congo kuendeleza maslahi yake madai ambayo Kigali inakanusha.

XS
SM
MD
LG