Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 04:35

Rwanda kuisaidia Benin kupambana na waasi wenye kufuata itikadi za kislamu


Watu watatu waliohusika na utekaji nyari katika shule ya sekondari ya Bethel Baptist wakionyeshwa kwa waandishi habari mjini Abuja, Nigeria.
Watu watatu waliohusika na utekaji nyari katika shule ya sekondari ya Bethel Baptist wakionyeshwa kwa waandishi habari mjini Abuja, Nigeria.

Rwanda huenda itaisaidia Benin kwa msaada wa uchukuzi ili kuweza kukabiliana na uasi unaongezeka unaofanywa na wanamgambo wa kislamu, ambao unatishia kanda zima ya Afrika Magharibi. Hii ni kulingana na msemaji wa rais ya Benin, Wilfried Leandre Houngbedji.

Akizungumza na shirika la habari la Reuters, Hougbedji amesema mazungumzo kati ya nchi yake na Rwanda yanaendelea kuhusu uwezekano wa kupata msaada wa kijeshi bila ya kuwahusisha wanajeshi wa Rwanda.


Benin na mataifa mengine ya Ghuba ya Guinea, Togo na Ivory Coast yanashuhudia kuongezeka kwa mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wenye uhusiano na makundi ya Al Qaeda na Islamic State, wakati ghasia hizo zikiongezeka kuelekea upande wa ksuini kutoka kanda ya Sahel.


Houngbedji anasema “nchi yake sawa na Niger na Burkina Faso iko katika majadiliano na serikali ya Rwanda juu ya msaada wa uchukuzi na wataalamu.”

Matamshi yake yametolewa baada ya ukurasa wa mtandao wa tasisi yenye makazi yake Paris juu ya masuala ya ujasusi barani Afrika, kuripoti kwamba serikali ya Cotonou iko katika majadiliano ya kupelekwa wanajeshi wa Rwanda ndani ya Benin ili kupambana na wanamgambo wa kislamu.

Kufuatana na makala hayo ni kwamba mazungumzo yako katika duru ya mwisho na kwamba kundi la kwanza la mamia ya wanajeshi na waatalamu wa Rwanda wanatarajiwa kuwasili Benin mwezi Oktoba.

Msemaji wa jeshi la Rwanda Ronald Rwivanga amesema hawezi kusema lolote kuhusu kuwepo kwa “ushirikiano wa ulinzi” kati ya Rwanda na Benin.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda kuzisaidia nchi za Afrika kupambana na waasi kwani tayari amewapeleka wanajeshi wake nchini Msumbiji, ili kupambana na waasi katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Cabo Delago na amepeleka wanajeshi wake kukabiliana na ghasia huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Makala haya inatokana na taarifa za mashirika ya habari ya Reuters na AFP

XS
SM
MD
LG