Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 14:33

Ruto aunda tume kuchunguza mauaji ya Shakahola


Jacob Inje akiwa na picha ya mpwa wake akisubiri kutoa sampuli ya DNA huko Malindi, tarehe 1 Mei 2023. Picha na SIMON MAINA / AFP.
Jacob Inje akiwa na picha ya mpwa wake akisubiri kutoa sampuli ya DNA huko Malindi, tarehe 1 Mei 2023. Picha na SIMON MAINA / AFP.

Rais wa Kenya William Ruto ameteua tume ya kuchunguza vifo vya zaidi ya watu 100 wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa dhehebu la kidini ambalo kiongozi wao aliwaamuru wakae na njaa, msemaji wa rais Ruto alisema.

Mamlaka nchini Kenya zinasema waliofariki walikuwa wanachama wa kanisa la Good News International lililokuwa likiongozwa na Paul Mackenzie, ambaye wanasema alitabiri mwisho wa dunia ungekuwa tarehe 15 Aprili na hivyo kuwaagiza wafuasi wake kujiua ili wawe wa kwanza kwenda mbinguni.

Idadi ya vifo imefikia 111, lakini inaweza kuongezeka zaidi, hii ni moja ya mafaa makubwa sana yanayohusiana na imani za kidini katika historia ya hivi karibuni.

Baadhi ya wabunge nchini Kenya wamezikosoa idara za usalama kwa kushindwa kuchukua fursa ya kuzuia vifo vya watu wengi vilivyotokea katika msitu wa Shakahola, baada ya kujulikana kuwa Mackenzie alikuwa amekamatwa mapema mwaka huu akituhumiwa kuhusika na mauaji ya watoto wawili ambao walikufa kwa njaa na kukosa hewa, na baadaye aliachiwa kwa dhamana.

Mackenzie, ambaye yuko chini ya ulinzi wa polisi, hajazungumza chochote hadharani juu ya tuhuma zinazomkabili na wala hajatakiwa kujibu shitaka lolote la jinai. Mawakii wawili wanaomwakilisha wamekataa kutoa maoni yao kwa shirika la habari la Reuters.

Mackenzie akiwa na washitakiwa wengine 17 walifikishwa mahakamani siku ya Ijumaa katika mji wa pwani wa Mombasa.

Akiitangaza tume hiyo, Msemaji wa rais Hussein Mohamed, alisema Ruto pia ameteua kikosi kazi kutathmini kanuni zinazosimamia taasisi za kidini.

Tume hiyo itaongozwa na jaji wa Mahakama ya Rufaa Jessie Lesiit na daktari wa magonjwa ya akili Frank Njenga na askofu Catherine Mutua ni miongoni mwa wajumbe wa tume hiyo.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habri la Reuters

XS
SM
MD
LG