Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:19

Maiti za waliokufa kwa imani za kidini Kenya zaendelea kufukuliwa


Ramani ya Kenya
Ramani ya Kenya

Idadi ya waathirika wanaoshukiwa kufa na njaa kutokana na imani za kidini nchini Kenya imeongezeka na kufikia 95 siku ya Jumatano, afisa wa serikali alisema, huku jamaa zao wakilia huku wakisubiri habari za wapendwa wao, baada ya wachunguzi kufukua makaburi ya jumla wiki iliyopita.

Kupatikana kwa dazerni ya miili iliyokuwa imezikwa katika msitu wa Shakahola karibu na mji wa pwani wa Malindi, uliwashtua wakenya, huku kiongozi wa dhehebu la kidini Paul Mackenzie Nthenge akishutumiwa kuwasukuma wafuasi wake kwa kuwahubiria kwamba kukaa na njaa ndiyo njia pekee ya kwenda kwa Mungu.

Sakata la kutisha, ambalo limepewa jina la "Mauaji ya Msitu wa Shakahola", limesababisha msako kwa vikundi vya kidini katika nchi hiyo yenye wakristo wengi.

"Tumechimba makaburi matano ambayo yanafikisha jumla ya idadi ya watu waliopoteza maisha kufikia 95," Rhoda Onyancha, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, aliwaambia waandishi wa habari.

Shirika la Msalaba Mwekundu limetoa msaada wa jokofu la kontena la kwenye lori ili kusaidia kuhifadhi baadhi ya maiti kwa kuwa Chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya serikali iliyopo katika Kaunti ya Malindi kilikuwa tayari kimejaa darzeni ya maiti ikiwa ni zaidi ya uwezo wake, huku familia zikiwa na hamu ya kufahamu kama wapendwa wao walikuwa wamepatikana.

Kijana Issa Ali alipelekwa Shakahola mwaka 2020 na mama yake, na aliliambia shirika la habari la AFP kuwa alikuwa akipigwa na Nthenge alipojaribu kuondoka, hadi baba yake alipomuokoa.

"Mara ya mwisho kumuona mama yangu ilikuwa mwezi Februari," mtoto huyo mwenye umri wa miaka 16 alisema kwa sauti ya upole.

"Alikuwa dhaifu sana mara ya mwisho nilipomuona."

Afisa wa Msalaba Mwekundu Kenya, Hassan Musa, aliliambia shirika la habari la AFP kuwa watu 311, wakiwemo watoto 150, wameripotiwa wamepotea huko Malindi.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP na Reuters

XS
SM
MD
LG