Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:15
VOA Direct Packages

Takriban miili 40 yapatikana ikiwa imezikwa kwenye shamba la mchungaji mwenye dhehebu lenye utata Kenya


Miili iliyofukuliwa kwenye kijiji cha Shakahola, karibu na Malindi, pwani ya kusini mwa Kenya, April 23, 2023.

Jumla ya miili 39 imepatika mwishoni mwa wiki kwenye shamba linalomilikiwa na mchungaji  mmoja, kwenye pwani ya Kenya, ambaye alikamatwa hivi karibuni kwa kuwaamuru wafuasi wake kufunga hadi kufa.

Mkuu wa polisi wa kaunti ndogo ya Malindi John Kemboi amesema Jumapili kwamba kuna makaburi zaidi ambayo yanahitaji kufukuliwa kwenye shamba hilo linalomilikiwa na mchungaji Paul Makenzi, aliyekamatwa Aprili 14 kutokana na uhusiano wake na dhehebu lenye utata.

Kufikia sasa jumla ya miili 43 imepatikana kwenye shamba hilo baada ya watu wanne wengine kufa muda mfupi baada ya kugundulika walikaa na njaa kwa muda mrefu kwenye kanisa la Good News International, wiki iliyopita. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Polisi wameiomba mahakama muda zaidi wa kumshikilia Makenzi kwa vile uchunguzi kuhusiana na vifo vya wafuasi wake unaendelea.

Ripoti kutoka kwa umma zilipelekea polisi kuvamia shamba la mchungaji lililopo Malindi ambako waliwagundua watu 15 waliokuwa dhaifu sana kutokana na njaa, wakiwemo wanne waliofariki muda mfupi baadaye. Wafuasi hao walisema kwamba walikaa na njaa kwa maelekezo ya mchungaji wao ili waweze kukutana na yesu.

Polisi walifahamishwa kulikuwa na darzeni ya makaburi yaliyotapakaa katika shamba la Makenzi, na kwa hivyo kuanza shughuli ya kuyafukua Ijumaa wiki iliyopita. Makenzi anasemakana alikuwa katika mgomo wa kula kwa muda wa siku nne zilizopita wakati akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Mchungaji huyo aliwahi kukamatwa mara mbili hapo awali, 2019 na Machi mwaka huu kuhusiana na vifo vya watoto. Kila wakati aliachiliwa kwa dhamana wakati kesi dhidi yake zikiwa zinaendelea mahakamani.

Wanasiasa wa eneo hilo wameisihi mahakama isimuachilie aendelee kushikiliwa kwa wakati huu, wakilalamikia kuongezeka kwa madhehebu ya aina hiyo kwenye eneo na Malindi.

XS
SM
MD
LG