Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 04:50

Ruto aanza ziara ya siku mbili Tanzania


Rais wa Kenya William Ruto (Kulia) akizungumza na Waziri wa Mambio ya Nje wa Tanzania Stergomena Lawrence Tax. Ameandamana na mkewe, Rachel Ruto na Waziri mteule wa Mambo ya Nje wa Kenya, Alfred Mutua.
Rais wa Kenya William Ruto (Kulia) akizungumza na Waziri wa Mambio ya Nje wa Tanzania Stergomena Lawrence Tax. Ameandamana na mkewe, Rachel Ruto na Waziri mteule wa Mambo ya Nje wa Kenya, Alfred Mutua.

Rais wa Kenya William Ruto aliwasili Tanzania Jumapili jioni kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Ruto atakutana na kufanya mashauri na Rais Samia Suluhu Hassan katika Ikulu jijini Dar es Salaam Jumatatu, ambapo wanatarajiwa kufanya mazungumzo.

Kulingana na taarifa ya serikali ya Tanzania, Rais Ruto atahutubia wanahabari kabla ya kushiriki chakula cha mchana katika Ikulu ya Tanzania.

Rais Ruto amesafiri katika mataifa kadhaa tangu kuapishwa kwake, ikiwa ni pamoja na Uingereza kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II, Marekani kuhudhuria Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Ethiopia kwa mazungumzo baina yake na Waziri Mkuu Abiy Ahmed, na Uganda ambako alihudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa nchi hiyo.

Hadi tukitayarisha ripoti hii ratiba rasmi ya kiongozi huyo haikuwa imewekwa wazi lakini wachambuzi wanasema ajenda kuu huenda itakuwa biashara kati ya mataifa hayo mawili.

Mauzo ya Kenya kwenda Tanzania yaliongezeka kwa asilimia 46 hadi dola milioni 236.7.

Mauzo ya Tanzania kwa Kenya kwa upande mwingine yalikua kwa asilimia 95.3 mwaka jana - karibu mara mbili hadi dola milioni 449.9 milioni mwaka 2021.

Ziara ya Ruto inajiri wakati yeye na Rais Samia Suluhu Hassan wakiahidi kuendelea kufanya kazi pamoja kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa watu wao na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Wakati wakuu hao wa nchi walipokutana Nairobi Septemba Mosi wakati wa kuapishwa kwa Ruto, rais huyo mpya aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema Serikali yake itashirikiana na Tanzania katika biashara, kilimo, usalama na maeneo mengine.

Kwa upande mwingine Rais Samia aliwapongeza Wakenya kwa kuonyesha ukomavu katika uchaguzi uliofanyika Agosti 9.

"Nataka kuwahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Kenya kuleta maendeleo," alisema Rais Hassan.

Ruto ameandamana na mkewe, Rachel Ruto na Waziri mteule wa Mambo ya Nje wa Kenya, Alfred Mutua.

XS
SM
MD
LG