Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 17:04

Russia yatangaza mpango wake kukamata maeneo ya kusini na mashariki ya Ukraine


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Jenerali wa Russia ametangaza Ijumaa kwamba Moscow inataka kukamata  maeneo yote ya kusini na mashariki mwa Ukraine ikiwa ni  malengo  mapana ya vita.

Hatuo hii mpya ni kinyume na ilivyokiri awali wakati ikiendelea na mashambulizi mapya baada ya kampeni yake ya kuuteka mji mkuu wa Kyiv kuvunjika mwezi uliopita.

Ukraine imesema maelezo yaliyotolewa na Rustan Minnekayev kamanda msaidizi wa wilaya kuu katika jeshi la Russia, yameonyesha uongo kwa madai ya hapo awali ya Russia kwamba haina malengo ya eneo.

Alinukuliwa na vyombo vya habari vya serikali ya Russia akisema kuwa Moscow inalengo la kuchukua eneo lote la mashariki la mkoa wa Donbas kuiunganisha na peninslula ya Crimea na upande wote wa kusini mwa Ukraine hadi eneo lililojitenga la Moldova linalokaliwa kimabavu na Russia.

Hi ikimaanisha kujiingiza kwa mamia ya maili zaidi kuliko ilivyo sasa, kupita katika miji mikubwa ya Ukraine ya Mykolaiv na Odesa.

XS
SM
MD
LG