Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 05:49

Russia imefanya jaribio la kombora la nuclear


Rais wa Russia Vladmir Putin katika mojawapo ya vikao na maafisa wa serikali yake mjini Moscow. PICHA: AFP
Rais wa Russia Vladmir Putin katika mojawapo ya vikao na maafisa wa serikali yake mjini Moscow. PICHA: AFP

Russia imefanya jaribio la kombora la nuclear, ambalo rais wa nchi hiyo Vladmir Putin amesema kwamba litawafanya maadui wa Moscow kukoma na kufikiria tena.

Jaribio hilo limefanyika miezi miwili tangu Russia ilipoivamia Ukraine.

Putin alionekana kwenye televisheni akiambiwa na wakuu wa jeshi kwamba kombora hilo la masafa marefu limefanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza.

Jaribio limefanyika kutoka Plesetsk, kaskazini magharibi mwa Russia na limepiga malengo katika Penisula ya Kamchatka, umbali wa karibu kilomita 6,000.

Jaribio hilo la kombora hata hivyo halikushutua nchi za magharibi, lakini limefanyika wakati kuna mivutano mikubwa ya kisiasa.

Russia haijadhibithi mji wowote mkubwa wa Ukraine tangu ilipotuma maelfu ya wanajeshi wake nchini Ukraine, Februari 24.

XS
SM
MD
LG