Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 10:04

Russia yashambulia kwa makombora karibu na mpaka wa Poland


Uharibifu uliotokana na shambulizi la Russia katika kituo cha kijeshi cha Yavoriv, wakati Russia ikiendelea na uvamizi wa Ukraine, Yavoriv, Lviv, Ukraine, Macih 13, 2022 (Picha kutoka mitandao ya kijamii @BackAndAlive/via REUTERS
Uharibifu uliotokana na shambulizi la Russia katika kituo cha kijeshi cha Yavoriv, wakati Russia ikiendelea na uvamizi wa Ukraine, Yavoriv, Lviv, Ukraine, Macih 13, 2022 (Picha kutoka mitandao ya kijamii @BackAndAlive/via REUTERS

Moja ya vituo vikubwa sana vya mafunzo ya kijeshi Ukraine, kilichopo kilomita 25 kutoka kwenye mpaka wa Poland, magharibi mwa nchi, kimeshambuliwa na makombora ya Russia na watu 35 wameuawa na wengine 134 wamejeruhiwa, kulingana na maafisa wa Ukraine.

Moja ya vituo vikubwa sana vya mafunzo ya kijeshi Ukraine, kilichopo kilomita 25 kutoka kwenye mpaka wa Poland, magharibi mwa nchi, kimeshambuliwa na makombora ya Russia na watu 35 wameuawa na wengine 134 wamejeruhiwa, kulingana na maafisa wa Ukraine.

Kituo hicho cha kijeshi kilichopo Yavoriv kipo kilomita 60 kutoka Lviv, kituo kikubwa cha kupokea wanaoondoka Ukraine kuelekea Poland. Pia kimetumiwa na wakufunzi wa kijeshi wa NATO, lakini maafisa wa Ukraine wanasema bado wanajaribu kufahamu iwapo kulikuwa na wakufunzi wowote katika kituo hicho wakati wa shambulizi hilo na kujeruhiwa.

Shambulizi hilo katika Kituo cha Kimataifa kwa Ajili Ulinzi wa Amani na Usalama ni shambulizi lkubwa lililofanyika upande wa magharibi lililofanywa na Russia hadi sasa na kuongeza wasiwasi kuwa Lviv inaweza haraka kuingia katika vita hiyo.

Kwa zaidi ya wiki moja iliyopita VOA iliripoti kuwa mashirika ya upelelezi ya Marekani yalikhofia Belarus, mshirika wa Russia na eneo ambalo Russia inalitumia kumvamia jirani yake, inaweza kupeleka wanajeshi wake kujiunga na vita hivyo, na huenda watafanya mashambulizi kaskazini magharibi mwa Ukraine na kati, na kuhatarisha usalama wa Lviv.

Hadi sasa Belarus haijaingia katika vita moja kwa moja na shambulizi katika kituo cha mafunzo ya kijeshi lilifanywa na Russia. Lakini maafisa wa Marekani na Ulaya wana wasiwasi na Belarus.

Ramani ya Ukraine ikionyesha iliko Lviv.
Ramani ya Ukraine ikionyesha iliko Lviv.

Mbali na hilo, tathmini ya kijasusi ilieleza kuwa Lviv isichukuliwe kuwa ni eneo salama. Ujumbe uliotumwa kwa taasisi zisizo za kiserikali na miradi inayofadhiliwa na Marekani na iliyoanyiwa tathmini ya kijasusi ilitahadharishwa : “Miji katika nchi za Magharibi haichukuliwi tena kuwa salama.” Wafanyakazi wa NGO walioko Ukraine wameshauriwa kuondoka Lviv na kutafuta hifadhi katika vijiji vya mpakani, ambavyo huenda havitakuwa vinalengwa na makombora.

Gavana wa eneo la mkoa wa Lviv alisema makombora 30 yalipiga kituo cha mafunzo ya kijeshi. Lakini maafisa wa serikali kuu wamekadiria ni makombora nane yalipiga kambi hiyo. “Wavamizi walifanya mashambulizi ya anga katika Kituo cha kimataifa cha Kulinda Amani na Usalama. Kulingana na takwimu za awali, walipiga makombora manane.,” Anton Mironovich, msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Ukraine, ameliambia shirika la habari la Interfax la Ukraine.

Mtu aliyejeruhiwa akiwasili katika hospitali ya mji wa Novoiavorisk, magharibi ya Ukraine baada ya Russia kushambulia Kituo cha Mafunzo ya Kijeshi magharibi ya Ukraine kinacho endesha mazoezi ya kijeshi ya NATO. western Ukraine, March 13, 2022. (AP Photo/Bernat Armangue)
Mtu aliyejeruhiwa akiwasili katika hospitali ya mji wa Novoiavorisk, magharibi ya Ukraine baada ya Russia kushambulia Kituo cha Mafunzo ya Kijeshi magharibi ya Ukraine kinacho endesha mazoezi ya kijeshi ya NATO. western Ukraine, March 13, 2022. (AP Photo/Bernat Armangue)

Kulengwa kwa Yavoriv inaonekana kwa baadhi ya wanadiplomasia wa Magharibi kama ujumbe wakiimarisha tahadhari iliyotolewa Jumamosi na naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Ryabkov, aliyesema misafara ya silaha ya nchi za Magharibi kuingia Ukraine inachukuliwa hivi sasa na Moscow kuwa “ni halali kulengwa na mashambulizi ya kijeshi.”

Kumekuwa na ongezeko hivi karibuni la mashambulizi ya anga yanayofanywa na Russia yakilenga vituo vya kijeshi huko magharibi mwa Ukraine. Wiki iliyopita mashambulizi mengine katika vituo vya ulinzi wa anga na viwanja vya ndege vya kijeshi magharibi mwa Ukraine, kilomita takriban 130 kusini mwa Lviv.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia Igor Konashenkov alisema Ijumaa kuwa majeshi ya Russia yamefanya mashambulizi ya makombora ya masafa marefu katika viwanja vya ndege viwili vya kijeshi katika miji ya magharibi mwa Ukraine ya Lutsk and Ivano Frankivsk.

Maafisa wa jeshi la Ukraine wamethibitisha mashambulizi hayo lakini wamekanusha madai ya Russia kuwa vifaa vya ulinzi wa anga katika vituo vyote vya ndege vilikuwa vimeharibiwa. Maafisa katika eneo wamesema wanajeshi wawili wa Ukraine waliuawa na watu sita walijeruhiwa katika kiwanja cha ndege cha kijeshi cha Lutsk.

Majeshi ya Russia yalishambulia tena kituo cha anga cha kijeshi huko Ivano-Frankivsk Jumamosi asubuhi. Meya wa jiji hilo, Ruslan Martsinkiv, amewasihi watu wanaoishi karibu na kituo hicho kuondoka.

Waziri wa ulinzi wa Ukraine ameliita shambulizi la anga la Russia katika mji wa Yavoriv ni “shambulizi la kigaidi.” Oleksii Reznikov aliandika katika Twitter: “Russia imekishambulia Kituo cha Kimataifa cha Ulinzi wa Amani na Usalama karibu na Lviv.

Wakufunzi wa kigeni wanafanyakazi hapa. Taarifa za waathirika hao zinatafutwa kuthibitisha kilichowapata. Hili ni shambulizi jipya la kigaidi kwa amani na usalama karibu na mpaka wa EU-NATO. Hatua lazima zichukuliwe kusitisha hili. Funga anga!”

XS
SM
MD
LG