Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 19:16

Wanajeshi wa kitengo cha anga Marekani wamepelekwa Poland


Mfano wa maeneo ya msituni mashariki mwa Poland kutoka mpaka wa Ukraine

Mamia ya wanajeshi kutoka kitengo cha anga namba 82 cha Marekani wamepelekwa katika milima ya msituni ya mashariki mwa Poland kilomita chache tu kutoka mpaka wa Ukraine.

Hilo linawaweka karibu na mashambulizi ya karibuni ya anga ya Russia kwenye maeneo yaliyolenga magharibi mwa Ukraine. Kikosi hicho ni sehemu ya idadi kubwa ya wanajeshi 5,000 wa Marekani waliotumwa Poland katika wiki za karibuni na ni nyongeza ya wanajeshi wa Marekani ambao tayari wako nchini humo.

NATO imesema vikosi hivyo vinatuma ujumbe kwa Moscow kwamba muungano huo utatetea kila nchi ya eneo lake. Hata hivyo kuna wasi-wasi unaoongezeka wa ushiriki wa bahati mbaya kati ya Marekani na Russia.

Njia za mawasiliano zimeanzishwa ili kuepuka hali hiyo. Pia kuna hofu kwamba wanajeshi wa NATO walioko mashariki mwa Ulaya wanaweza kulengwa iwapo matukio yanaongezeka.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG