Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 09:02

Wabunge Marekani wanaahidi kutoa msaada zaid wa kijeshi kwa Ukraine


Chris Murphy, Seneta wa jimbo la Connecticut nchini Marekani
Chris Murphy, Seneta wa jimbo la Connecticut nchini Marekani

Siku moja baada ya wengi kuzungumza na Rais wa Ukraine, wabunge wa Marekani wanaahidi kutoa msaada wa ziada wa kijeshi kwa Kyiv, wakati serikali ya huko ikiendelea kupigania uhai wake kufuatia uvamizi wa Russia.

Bunge hivi karibuni litaidhinisha ufadhili wa dharura, na kuweka dola bilioni 10 katika vifaa vya ulinzi kwa Ukraine, lakini pia misaada ya kibinadamu ili kuwaondoa raia alisema seneta Chris Murphy wa jimbo la Connecticut kwenye kituo cha televisheni cha Fox News siku ya Jumapili.

Licha ya uungwaji mkono wa pande zote na msaada wenye nguvu kuisaidia Kyiv, wabunge waangalia ombi jingine la Ukraine; eneo marufuku ya kutumia anga ya nchi ili kuzuia mashambulizi ya anga ya Russia. Hiyo itamaanisha vita vya tatu vya Dunia, seneta wa Republican, Marco Rubio wa jimbo la Florida aliiambia program ya This Week katika televisheni ya ABC siku ya Jumapili. “Nadhani kuna mambo mengi tunaweza kufanya ili kuisaidia Ukraine kujilinda, lakini nadhani watu wanahitaji kuelewa maana ya marufuku ya anga”.

Seneta mwingine Joe Manchin wa jimbo la West Virginia, m-Democrat alielezea msimamo wa wastani. Sitapinga chochote kilichopo mezani, alisema kwenye kipindi cha “Meet the Press” cha NBC.

XS
SM
MD
LG