Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:23

White House haikubaliani na wito wa Seneta uanotaka Putin auwawe


 Seneta Lindsey Graham (kushoto) na Rais wa Russia Vladimir Putin (Photo by Andrew CABALLERO-REYNOLDS and Andreas SOLARO / AFP)
Seneta Lindsey Graham (kushoto) na Rais wa Russia Vladimir Putin (Photo by Andrew CABALLERO-REYNOLDS and Andreas SOLARO / AFP)

Uongozi wa Biden hautetei mapinduzi nchini Russia, White House imesema Ijumaa, baada ya seneta wa Marekani kuwataka raia wa Russia kumuua Rais Vladimir Putin.

Uongozi wa Biden hautetei mapinduzi nchini Russia, White House imesema Ijumaa, baada ya seneta wa Marekani kuwataka raia wa Russia kumuua Rais Vladimir Putin.

“Huo siyo msimamo wa serikali ya Marekani na bila shaka siyo tamko utalisikia kutoka – kinywani – mwa yeyote anayefanya kazi na utawala huu,” Msemaji wa White House Jen Psaki amewaambia waandishi akijibu swali kutoka Sauti ya Amerika.

Seneta wa Marekani Lindsey Graham, Mrepublikan kutoka South Carolina, alipendekeza katika mahojiano yake kwa njia ya televisheni Alhamisi jioni kuwa “mtu mmoja Russia” anatakiwa amuuwe Putin. Alirejea matamshiyake hayo Ijumaa katika mahojiano mengine na kituo cha televisheni cha Fox News.

“Vipi hili litamalizika? Mtu mmoja nchini Russia lazima asimame kulitekeleza … na kumuondoa jamaa huyu,” Graham amemwambia mwandishi Sean Hannity wa Fox News aliyekuwa akimhoji.

Baada ya mahojiano hayo, Graham aliweka ujumbe katika Twitter, “Watu pekee wanaweza kulitatua hili ni wananchi wa Russia.”

“Je yuko mfano wa Brutus nchini Russia? Je, yuko ambaye ni shujaa aliyefanikiwa zaidi mfano wa Kanali Stauffenberg katika jeshi la Russia? Seneta aliandika. Marcus Junius Brutus alimuua mtawala wa Rome Julius Caesar, wakati Afisa wa Jeshi la Ujerumani Claus von Stauffenberg alijaribu bila mafanikio kumuua kiongozi wa Ujerumani Adolf Hitler mwezi Julai 1944.

Balozi wa Russia nchini Marekani, Anatoly Antonov, amesema matamshi ya Graham “hayakubaliki na yanaghadhibisha” na alisema yanaelezea chuki “iliyovuka mipaka” nchini Marekani dhidi ya Russia.

Alidai “maelezo rasmi na shutuma kali kwa taarifa za kihalifu.”

Wabunge wa Marekani, wa upande wa Wademokrat na Warepublikan, pia walimkosoa Graham kwa maoni yake hayo.

Seneta Mrepublikan wa Texas Ted Cruz ameliita pendekezo la Graham “wazo baya la kipekee,” wakati Mwakilishi Mdemokrat Ilhan Omar wa Minnesota alituma ujumbe wa Tweet: “Natamani wabunge watulie kidogo na kuchunga matamshi yao wakati utawala huu unashughulika kuepusha vita ya tatu ya dunia.

Graham alileta azimio katika bunge la kulaani vitendo vya “uhalifu wa kivita” na uhalifu dhidi ya binadamu vinavyofanywa na Putin na makamanda wake wa kijeshi huko Ukraine.

Baadhi ya taarifa hizi zimetoka shirika la habari la AP na AFP.

XS
SM
MD
LG