Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:32

Russia inasema inafungua njia watu kuondoka katika miji miwili ya Ukraine


Igor Konashenkov (REUTERS/Maxim Zmeyev - D1BEUDNILNAA)
Igor Konashenkov (REUTERS/Maxim Zmeyev - D1BEUDNILNAA)

Russia inasema inasitisha mapigano katika miji miwili ya Ukraine kuruhusu wakazi wa maeneo hayo kuondoka.

Msemaji wa Wizara wa Ulinzi ya Russia Igor Konashenkov alisema, “Leo, Machi 5, kuanzia saa nne asubuhi kwa saa za Moscow, upande wa Russia umetangaza kusitisha mapigano na kufungua njia za misaada ya kibinadamu kuruhusu raia kuondoka Mariupol na Volnovakha. Njia za misaada ya kibinadamu na njia za kutoka zimekubaliwa na upande wa Ukraine.”

Njia hiyo kutoka Mariupol zitafunguliwa kwa a saa tano, wizara imewakariri maafisa wa mji wakisema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema majeshi ya Russia “yanaendelea kutumia mbinu za kikatili nchini Ukraine, ikiwemo kuwashambulia raia.”

Maoni yake yalifuatiwa na shambulizi la Russia katika kinu cha nyuklia Ukraine – kinu kikubwa cha aina yake Ulaya – ambacho kilisababisha moto ndani ya jengo la kinu hicho.

Akizungumza na waandishi Ijumaa kabla ya mkutano wake na wenzake wa Umoja wa Ulaya huko Brussels, Blinken alisema, “Tunakabiliwa sote na kile ambacho ni vita alivyochagua Rais [Vladimir] Putin: havijachochewa, havina uhalali, na vita ambayo vinatisha, vyenye matokeo ya kutisha.”

“Sisi tuna nia ya dhati kufanya kila kitu tunachoweza kufanya kusitisha hili,” aliongeza, lakini alifuta uwezekano wa kuweka marufuku ya ndege zisiruke huko Ukraine, akisema hatua hiyo inaweza kupelekea vita kubwa zaidi.

“Tuna jukumu kuhakikisha vita hii havivuki mipaka ya Ukraine. … Kuweka marufuku ya anga inaweza kupelekea vita kamili ndani ya bara la Ulaya,” amesema.

Mkutano uliofanyika Brussels umefanyika baada ya Ukraine kuishutumu Russia na “tishio la nyuklia” kwa kupiga mabomu na kusababisha moto katika kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia kabla ya kukidhibiti kinu hicho. Kinu hicho kiko katika mji wa Enerhodar upande wa kusini mashariki wa nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG