Nemtsov alipigwa risasi na kuuwawa mwaka 2015 karibu na Kremlin.
Hayati Nemtsov Aliyewahi kuwa naibu waziri mkuu chini ya Rais wa zamani Boris Yeltsin, alikuwa mwanasiasa maarufu na mkosoaji mkali wa Rais Vladimir Putin.
Usiku wa Februari 2015, alipigwa risasi na washambuliaji kwenye daraja karibu na Kremlin alipokuwa akitembea na mpenzi wake, kifo chake kililishtua Taifa Hilo.
Wanaume watano kutoka mkoa wa Chechnya nchini Russia walipatikana na hatia kwa mauaji yake, huku mshambuliaji akipewa adhabu ya kifuno cha miaka 20.
Lakini washirika wa Nemtsov waliitaja adhabu hiyo kuwa jaribio la kuondoa lawama kutoka kwa serikali.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.
Forum