Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 02, 2024 Local time: 09:06

Oleg Orlov amehukumiwa miaka miwili na nusu jela huko Moscow


Oleg Orlov, mwanaharakati mkongwe wa haki za binadamu
Oleg Orlov, mwanaharakati mkongwe wa haki za binadamu

Orlov mwenye miaka 70 amehudumu zaidi ya miongo miwili katika kundi la haki za binadamu la Memorial

Mwanaharakati mkongwe wa haki za binadamu Oleg Orlov amehukumiwa Jumanne na mahakama ya Moscow kifungo cha miaka miwili na nusu jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuyadhalilisha majeshi ya Russia katika kesi ambayo imelaaniwa na waangalizi wa kimataifa wakieleza ina ushawishi wa kisiasa.

Orlov, mwenye umri wa miaka 70, amehudumu kwa zaidi ya miongo miwili kama mmoja wa viongozi wa kundi la haki za binadamu la Memorial. lilishinda sehemu ya Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2022, mwaka mmoja baada ya kupigwa marufuku na kufutwa nchini Russia.

Taarifa ya kundi la Memorial ilisema Orlov alifungwa pingu baada ya hukumu hiyo, na mahakama iliamuru mara moja awekwe chini ya ulinzi. Katika maelezo yake ya mwisho kwenye kesi hiyo Jumatatu, Orlov alishutumu kuminywa kwa uhuru nchini Russia, ambapo alielezea kama udhaifu katika mahakama.

Kesi dhidi yake ilitokana na makala aliyoandika mwaka 2022 ambapo alisema Russia chini ya Rais Vladimir Putin imetumbukia katika ufashisti.

Forum

XS
SM
MD
LG