Jeshi la angani la Ukraine limesema kwamba mfumo wa ulinzi wa anga umeharibu ndege zisizokuwa na rubani 13 kati ya 19 zilizorushwa, pamoja na makombora sita.
Ndege zisizokuwa na rubani zilikamatwa kwenye anga ya maeneo ya Kharkiv, Dnipropetrovsk, Zaporizhzhia na Donetsk.
Gavana wa Dnipropetrovsk, Serhiy Lyasak, ameandika ujumbe kwenye Telegram kwamba ndege zisizokuwa na rubani zilianguzhwa katika wilaya mbili tofauti na kwamba makombora ya Russia pia yalilenga eneo hilo.
Lysak amesema kwamba hakuna majeruhi yameripotiwa.
Pentagon imesema kwamba waziri wa ulinzi wa marekani Lyoyd Austin na mwenzake wa Ukraine Rustem Umerov, wamafanya mazungumzo kwa njia ya simu jana Jumanne, kuhusu vita vya Ukraine.
Austin amesisitiza kwamba Marekani na washirika wake wataendelea kusaidia Ukraine wakati vita hivyo vinaingia mwaka wa pili.
Forum