Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 27, 2025 Local time: 12:16

Russia haitafaidika kwa kuzuia biashara kupitia bahari ya Black Sea -Uingereza


Moja ya bandari za Black Sea.
Moja ya bandari za Black Sea.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumamosi katika taarifa yake ya kijasusi ya kila siku kuhusu uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine kwamba Russia haitanufaika na kuzuiliwa kwa biashara yoyote kwelekea Ukraine kupitia bahari ya Black Sea.

Biashara ya kusafirisha bidhaa kupitia bahari ya Black Sea imesalia imara kwa kiasi kikubwa, taarifa hiyo ilisema lakini ikaongeza kuwa hatari inayoweza kutokana na kushindwa kijeshi, na "matokeo mabaya ya kisiasa" ya Russia kushambulia meli za wafanyabiashara, zinaweza kuwa na "athari kubwa zaidi kuliko" faida yoyote kutoka kwa kizuizi cha biashara inayoenda Ukraine.

Ikulu ya Marekani iliishutumu Korea Kaskazini siku ya Ijumaa kwa kusafirisha silaha hadi Russia, karibu na mpaka wa Ukraine.

Madai yake yanatokana na picha iliyotolewa Ijumaa inayoonyesha shehena kutoka bohari ya mizigo nchini Korea Kaskazini, au DPRK, ambayo ilipakiwa kwenye meli iliyokuwa na bendera ya Russia kabla ya kuhamishwa kwa njia ya reli hadi kwenye bohari kando ya mpaka wa kusini magharibi mwa Russia.

Uwasilishaji huo ulifanyika kati ya Septemba 7 na Oktoba 1, Marekani inasema.

Forum

XS
SM
MD
LG