Stoltenberg, pia anatoa wito kwa washirika kutoa misaada zaidi, kuongeza utengenezaji wa silaha na kuharakisha uwasilishaji wa silaha kwa Ukraine.
Akizungumza na wanahabari mjini Kyiv, amesema kadri Ukraine, inavyozidi kuwa na nguvu, ndivyo uvamizi wa Russia unakaribia kumalizika.
Akizungumza pamoja na rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, Stoltenberg amesema NATO imeshatoa oda ya silaha zenye thamani ya dola bilioni 2.5 kupelekwa Ukraine.
Stoltenberg amesema ni kwa maslahi ya usalama ya NATO kuipa Ukraine kile inachohitaji kushinda vita hivyo.
Na nchini Marekani, ambako serekali inatarajiwa kufungwa, msemaji wa Pentagon, Sabrina Singh, amesema juhudi za kusaidia vita vya Ukraine zinaweza kutatizwa.
Forum