Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Kiir na Putin walikutana mjini Moscow na kujadili masuala ya siasa na usalama nchini Sudan Kusini, ambayo inajitayarisha kufanya uchaguzi wake wa kwanza wa rais Decemba mwaka ujao.
Taifa hilo lilipata uhuru wake kutoka Sudan 2011, na tangu wakati huo, Kiir amekuwa kiongozi wake. Kulingana na video iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii na Kremlin ya viongozi hao wakitoa taarifa zao kwa umma, Putin alisema kwamba maendeleo kwenye viwanda vya kusafisha mafuta Sudan Kusini kwa kushirikiana na makampuni ya Russia kutaimarisha ushusiano wao.
Mwaliko wa Kiir nchini Russia umekuja wakati mataifa yenye nguvu ulimwenguni yakifikia mataifa ya kiafrika ili kupata uungaji mkono dhidi ya uvamizi wa Russia nchini Ukraine. Sasa hivi kampuni ya Russia ya Safinat inatengeneza kiwanda cha kusafishia mafuta kwenye jimbo la Unity la Sudan Kusini.
Forum