Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 09:53

Rusesabagina ataachiliwa huru Jumamosi - Serikali ya Rwanda

PICHA YA MAKTABA: Paul Rusesabagina (Kulia).
PICHA YA MAKTABA: Paul Rusesabagina (Kulia).

Paul Rusesabagina, ambaye alionyeshwa kama shujaa katika filamu ya Hollywood "Hotel Rwanda" na anatumikia kifungo cha miaka 25 kwa tuhuma za ugaidi, ataachiliwa Jumamosi, msemaji wa serikali ya Rwanda alisema Ijumaa.

Rusesabagina alihukumiwa Septemba 2021 kutokana na uhusiano wake na kundi linalopinga utawala wa Kagame. Alikanusha mashtaka yote na kukataa kushiriki katika kesi hiyo ambayo yeye na wafuasi wake walidai imechochewa kisiasa.

Tangazo la kuachiliwa kwake linafuatia shinikizo la kidiplomasia la Marekani, ambako Rusesabagina ana haki ya ukazi wa kudumu.

Kihistoria uhusiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili umekuwa mbaya kwa sababu ya kesi hiyo, na juu ya madai ya Rwanda kuingilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mfanyabiashara huyo wa zamani alisema kwamba yeye alikuwa kiongozi wa chama cha Rwanda Movement for Democratic Change lakini hakuwa na jukumu lolote katika mrengo wa kijeshi wa kundi hilo la National Liberation Front ambalo lilifanya mashambulizi.

Wakati hukumu yake ya miaka 25 gerezani ilipotolewa na mahakama, aendesha mashtaka waliitaja kuwa nyepesi mno.

Familia yake imekuwa ikishinikiza kuachiliwa kwake, ikisema alikuwa mgonjwa. Rusesabagina aliwaokoa takribani watu 1,200 kwa kuwahifadhi katika hoteli wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo zaidi ya watu laki nane waliuawa.

Kuachiliwa kwa mfanyabiashara huyo wa zamani wa hoteli kunaweza kusaidia kupunguza mvutano kati ya Rwanda na Marekani, ambayo mara kwa mara imekuwa ikiitaka Rwanda kusitisha uungaji mkono wake kwa kundi la waasi la M23 na kuwaondoa wanajeshi wake katika nchi jirani ya Kongo. Rwanda inakanusha kuhusika na Kongo.

Rusesabagina anatarajiwa kuachiliwa pamoja na wengine 19, ambao hukumu zao pia zilibadilishwa kwa amri ya rais baada ya maombi ya kuhurumiwa, msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo aliambia Reuters.

Wakati hukumu yake ya miaka 25 gerezani ilipotolewa na mahakama, aendesha mashtaka waliitaja kuwa nyepesi mno.

Familia yake imekuwa ikishinikiza kuachiliwa kwake, ikisema alikuwa mgonjwa. Rusesabagina aliwaokoa takribani watu 1,200 kwa kuwahifadhi katika hoteli wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo zaidi ya watu laki nane waliuawa.

Kuachiliwa kwa mfanyabiashara huyo wa zamani wa hoteli kunaweza kusaidia kupunguza mvutano kati ya Rwanda na Marekani, ambayo mara kwa mara imekuwa ikiitaka Rwanda kusitisha uungaji mkono wake kwa kundi la waasi la M23 na kuwaondoa wanajeshi wake katika nchi jirani ya Kongo. Rwanda inakanusha kuhusika na Kongo.

Rusesabagina anatarajiwa kuachiliwa siku ya Jumamosi pamoja na wengine 19, ambao hukumu zao pia zilibadilishwa kwa amri ya rais baada ya maombi ya kuhurumiwa, msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo aliambia Reuters.

XS
SM
MD
LG