Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:54

Kagame: Majadiliano yanaendelea kusuluhisha hatma ya Rusesabagina


Paul Rusesabagina, akitembea amefungwa pingu akielekea mahakamani mjini Kigali, Februari 26, 2021.

Rais wa Rwanda Paul Kagame leo amesema kuna majadiliano yanayoendelea juu ya kusuluhisha hatma ya Paul Rusesabagina ambaye alionyeshwa kama shujaa katika filamu ya Hollywood “Hotel Rwanda” na anatumikia kifungo cha miaka 25 jela nchini Rwanda kwa mashtaka ya ugaidi.

Rusesabagina alihukumiwa mwezi Septemba mwaka wa 2021 kutokana na uhusiano wake na kundi linalopinga utawala wa Kagame. Alinakusha mashtaka yote na kukataa kushiriki katika kesi hiyo ambayo yeye na wafuasi wake waliitaja kuwa imechochewa kisiasa.

Washington ilimtaja Rusesabagina kama ‘mfungwa anayezuiliwa kimakosa”, kwa kile ilichokiita ukosefu wa kesi ya haki. Rusesabagina ana haki za mkazi wa kudumu wa Marekani.

Kagame alisema nchi yake haikotubali kushinikizwa juu ya Rusesabagina, lakini leo Jumatatu ameonekana kusema kuwa kuna nafasi ya maelewano.

“Hatutaki kukwamishwa na yaliyopita. Tunasonga mbele,” Kagame amesema katika mahojiano na Jukwaa la Global Security.

“Kwa hiyo kuna majadiliano, kuna kuangalia njia zote zinazowezekana kutatua suala hili bila kuathiri mambo ya msingi ya kesi hiyo.

XS
SM
MD
LG