Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:03

Wawili wafariki baada ya basi lao kushambuliwa kwa risasi Rwanda


Basi mjini Kigali, Rwanda.
Basi mjini Kigali, Rwanda.

Watu wawili wameuawa na sita kujeruhiwa wakati watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo walipofyatulia risasi basi kusini magharibi mwa Rwanda, karibu na mpaka na nchi jirani ya Burundi, polisi wa Rwanda wamesema.

Shirika la habari la Reuters linamenukuu taarifa ya polisi iliyoeleza kwamba shambulizi hilo, ambalo lilishababisha vifo vya dereva wa basi na abiria, lilitekelezwa na National Liberation Front (FLN), tawi la waasi la Movement for Democratic Change (MRCD) linalopinga serikali.

Polisi wamesema wanawasaka watu waliovamia basi hilo katika barabara ya Nyambage-Rusizi, katika msitu wa Nyungwe.

Serikali inasema FLN ilianzisha mashambulizi kutoka eneo la msitu wa Nyungwe karibu na mpaka wa Burundi mwaka wa 2018.

Mwezi Aprili, serikali ya Rwanda iliidhinisha kifungo cha miaka 25 jela kwa Paul Rusesabagina, ambaye alionyeshwa kwenye sinema ya "Hotel Rwanda" akiwahifadhi mamia ya watu wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994, kwa kuhusika kwake na MRCD.

Alihukumiwa mwezi Septemba mwaka jana, baada ya kupatikana na hatia kwa mashtaka nane ya ugaidi, ambayo ameyakanusha.

XS
SM
MD
LG