Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 03, 2023 Local time: 04:50

RSF yaitaka China kutowafukuza waandishi wa gazeti la Wall Street


Geng Shuang
Geng Shuang

Waandishi wa habari bila mipaka (RSF) Ijumaa wameitaka China kusitisha uamuzi wake wa kuwafukuza waandishi watatu wa gazeti la Wall Street wanaofanyia kazi Beijing baada ya serikali ya nchi hiyo kulaani makala yenye maoni iliyochapishwa na gazeti la New York kuwa ni la “ubaguzi wa rangi.”

Kufukuzwa kwa waandishi hao watatu kumekuja siku moja baada ya serikali ya Marekani kuorodhesha vyombo vitano vya habari vya serikali ya China vilivyoko Marekani kama ni ofisi za ubalozi wa China kwa sababu vinatumika kama wasemaji wanaofanya juhudi ya kusambaza propaganda za serikali ya China.

Wakosoaji wanasema hatua ya China ni ukiukaji wa kushtusha wa uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujielezea wakati ikipeleka tishio kwa waandishi ambao bado wanafanya kazi huko China.

Na hilo linaweza kufikia kuharibu taswira ya China na kuchochea hisia hasi dhidi ya China ulimwenguni, wakosoaji wamefafanua.

“Huu ni uamuzi ambao hauwezi kuhalalishwa kabisa katika hali yoyote. Waandishi hao watatu waliofukuzwa na China hawahusiki kwa namna yoyote na makala hiyo ya maoni… Na kwa hiyo, hakuna sababu kabisa kuwa wao waadhibiwe kwa hilo,” amesema Cedric Aliviani, mkuu wa ofisi ya RSF Asia huko Taipei.

Kufukuzwa kwa waandishi hao watatu kulitangazwa Jumatano na msemaji wa wizara ya mambo ya nje Geng Shuang, aliyesema makala hiyo ya maoni ya gazeti hilo, iliyokuwa na kichwa cha habari “China is the real sick man of Asia,” lilikuwa ni chapisho “la ubaguzi wa rangi” na kichwa cha habari cha “udaku.”

Wakati akilikosoa gazeti hilo kwa kushindwa kuomba msamaha, Geng alisema wizara hiyo imeamrisha waandishi hao watatu, naibu msimamizi wa ofisi Josh Chin na waandishi Chao Deng na Philip Wen – kuondoka China ifikapo Jumapili. Chin na Deng ni raia wa Marekani wakati Wen ni raia wa Australia.

Watatu hao hawakuhusika na chochote katika chapisho hilo la maoni, lililokuwa limeandikwa na Profesa wa Chuo Kikuu cha Brand Walter Russel Mead.

Katika Makala hiyo ya maoni, Mead alikuwa anakosoa namna China ilivyo shughulikia mlipuko wa virusi vya corona vijulikanavyo kama COVID – 19 na juhudi zilizo kuwa “hazina tija”, pamoja na hatari zinazolikabili soko la fedha la nchi hiyo. Geng hakusema iwapo serikali ya China ilikuwa imekasirishwa na ukosoaji huo.

XS
SM
MD
LG