Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 10:01

Martekani ina nia ya kuimarisha ushirikiano na Afrika: Pompeo


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo na mkewe Susan wakiwasili Dakar, Senegal

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo anakutana na Rais Macky Sall wa Senegal kwa mazungumzo yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa usalama na kupanua uhusiano wa kiuchumi.

Pompeo aliwasili Senegal Jumamoasi kuanza ziara yake ya kwanza ya nchi za Afrika tangu kuchukua wadhifa huo miaka miwili ilyopita na anatazamia kuzungumzia namna ya kuongeza ushawishi wa Marekani katika biashara, ukuwaji wa kiuchumi na uwekezaji na nchi za Afrika ili kushindana na Uchina na Rashia.

Alipowasili hapo jana mwana diplomasia mkuu wa Marekani amesema “tunaichukulia Senegal kama nanga ya demokrasia na usalama Afrika Magharibi.”

Marekani inaichukulia Senegal kama mshirika nyeti katika juhudi za Washington kudumisha Amani na usalama Afrika Magharibi na dunia kwa jumla.

Washington imetumia zaidi ya dola milioni 106 kwa ajili ya msaada wa usalama ili kusiadia taasisi za usalama za Senegal tangu 2014.

Kupitia wizara ya ulinzi, Marekani imesaidia kutoa mafunzo na vifaa kwa vikosi vya jeshi na polisi vya Senegal ili kupambana na kitisho kinachongezeka cha ugaidi na ghasia zinazoendelea katika kanda ya Sahel.

Ziara yake ya Senegal ina malizika Juamtatu jioni na ataelekea Lunda, mji mkuu wa Angola na kumaliza ziara yake mjini Addis Ababa Ethopia. Katika ziara hii yake atazitembelea pia Saudi Arabia na Oman kabla ya kurudi Washington baada ya ziara hiyo ya siku tisa.

Akiwa Luanda atakutana na Rais Joao Lourenco na waziri wa mambo ya kigeni Manuel Augusto kuthibitisha tena uungaji mkono wa Marekani katika juhudi za Angola kupambana na rushwa na kuimarisha demokrasia.

Mjini Addis Ababa, Pompeo atakutana na waziri mkuu Abiy Ahmed na rais Sahle-Work Zewde ka mazungumzo juu ya juhudi za pamoja kuhamasisha usalama wa kikanda na kusaidia ajenda ya mageuzi ya kisiasa na kiuchumi ya serikali ya Ethopia.

Akiwa Munich kwa mkutano wa Usalama Duniani Pompeo amezionya nchi za Afrika katika kukubali uwekezaji wa China.

“Ni rahisi kweli kuvutiwa na fedha zinazopatikana kwa urahisi, lakini tunafahamu madhara yake. Kwa pamoja tunaweza kufanya kazi bora zaidi. Makampuni ya nchi za magharibi yanafahamika kufanya chini ya misingi inayoleta mikataba mizuri na kazi nzuri.” amesema Pompeo.

Pompeo anataka kuonesha kwamba dhana kua taifa kuu la dunia halina mkakati maalum kwa Afrika ni uwongo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG