Rais huyo alikuwa chini ya kifungo cha nyumbani katika siku za nyuma.
Aziz ambaye aliongoza taifa hilo la kaskazini magharibi ya Afrika kuanzia mwaka 2008 mpaka 2019, amekuwa chini ya uchunguzi kwa mashitaka yanayo jumuisha utakatishaji fedha toka mwezi Machi mwaka 2021.
Rais wa zamani huyo amepinga shutuma hizo na kudai kwamba mashitaka hayo yamechochewa na sababu za kisiasa.
Amepinga vilevile kushiriki katika uchunguzi dhidi yake kwa kusema katiba inamlinda kutoshitakiwa akiwa yeye ni rais wa zamani.
Chanzo cha Habari : AFP