Katika ujumbe wake amesema ameeleza masikitiko yake na kutoa rambirambi za dhati kwa familia za wahathiriwa.
Ajali hiyo inayotajwa kua mbaya zaidi katika taifa hilo la Afrika ya kaskazini kwa zaidi ya muongo mmoja ilitokea wakati basi la abiria kugongana uso kwa uso na gari la kubeba mizigo na kuwaka moto katika kijiji kusini mwa nchi hiyo.
Ripoti za vyombo vya habari vya Algeria zinasema kwamba miili ya watu iliyoungua moto imetolewa kenye mabaki ya basi.
Ajali imetokea karibu na mji wa Outoul, kilomita 20 magharibi mwa Tamanrasset, katika jangwa la Sahara na umbali wa karibu kilomira 2, 000 kusini mwa mji mkuu wa Algiers.
Basi lilikuwa linasafiri kutoka mji wa Tamanrasset kuelekea Adrar. Wakaazi wa eneo hilo waliliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu kuwa basi hilo lilikuwa likiwashusha abiria na lilikuwa limekaribia kumaliza safari yake wakati lori aina ya Toyota lilipoligonga basi hilo.
Afisa wa kikosi maalum cha polisi Samir Bouchehit alisema lori hilo lilikuwa limebeba makopo ya petroli na likiendesha upande wa pili wa barabara.
Forum