Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 22:32

Wahamiaji zaidi ya 600 katika mipaka ya jangwa na Libya wanapatiwa misaada


Wahamiaji nchini Tunisia kwenye maeneo ya mipaka na jangwa na Libya

Mamia ya wahamiaji kutoka nchi za kusini mwa jangwa la Sahara walikimbia au kulazimishwa kuondoka Sfax baada ya mivutano ya ubaguzi wa rangi kuzuka kufuatia mauaji ya Julai 3 ya raia mmoja wa Tunisia kwenye mzozo kati ya wenyeji na wahamiaji.

Zaidi ya wahamiaji 600 waliolazimishwa kuondoka bandari ya Sfax nchini Tunisia hadi kwenye maeneo ya mipaka ya jangwa na Libya wanapewa hifadhi na misaada ya kibinadamu, Shirika la Hilali Nyekundu limesema Jumatano.

Hata hivyo makundi madogo ya watu bado yamekwama karibu na mipaka na Algeria na Libya. Mamia ya wahamiaji kutoka nchi za kusini mwa jangwa la Sahara walikimbia au kulazimishwa kuondoka Sfax baada ya mivutano ya ubaguzi wa rangi kuzuka kufuatia mauaji ya Julai 3 ya raia mmoja wa Tunisia kwenye mzozo kati ya wenyeji na wahamiaji.

Sfax ni kituo cha kuondokea kwa wahamiaji wengi kutoka nchi maskini na zilizokumbwa na ghasia wakiwa na matumaini ya kupata maisha bora huko Ulaya. Wengi wa wale waliofukuzwa kutoka Sfax waliachwa wakiwa katika hali ngumu kwenye jangwa karibu na mipaka ya Tunisia.

Forum

XS
SM
MD
LG